Posts

190. SIKU NILIPOKUWA DHAMBINI

Siku nilipokuwa dhambini, Nikaambiwa juu ya Mwokozi; Nikasikiliza na furaha, Kufahamu kwamba nitaokoka.     Niliambiwa Yesu apenda,     Aliyenifia Msalaba;     Dhambi zangu ataziondoa,     Nikaambiwa Yesu apenda. Tangu nilipoonja upendo, Yesu hukaa ndani ya moyo; Humu dunia ni kama mbingu, Kwani Kumjua Mwokozi ni tamu. Ili kazi nimfanyie Bwana; Maneno hayo ninayataja, Ninatembea pamoja naye, Hapo ndipo furaha siku zote.

191. SIKU KWA SIKU, BWANA NILINDE

Siku kwa siku, Bwana nilinde, Ili nikuamini ko kote; Gizani, mwangani, haidhuru, Nitaujua wema wa Mungu.     Kuamini, kuamini,     Nipate nguvu za kuamini;     Ijapokuwa taabu nyingi,     Nipate fadhili ya kuamini. Nisiogope mambo ya kesho, Nitapokea neema yako; Yote ambayo yatanijia, Nijue kwamba umenipenda. Siku kwa siku nikuamini, Nitakuona kwako mbinguni; Nikiteswa humu duniani, Hapo nitazidi kuamini.

192. MWOKOZI NIONGOZWE

Mwokozi niongozwe Nisipotee kamwe; Nina salama kwako, Nikae nawe pako.     Yesu, Yesu,     Niongoze nisipotee;     Maisha yangu yote,     Mwokozi unishike. Ee, kimbilio langu, Wakati dhoruba kuu; Nina salama yako Kutegemea kwako. Mwokozi unishike, Hata nichukuliwe; Mpaka nchi ya mwanga, Mle chozi hapana.

193. KATIKA YESU SINA SHAKA

Katika Yesu sina shaka, Yeye amenitosha; Pendo lake lanipendeza, Kwake nina ushirika. Katika Yesu sina shaka, Amenilinda po pote; Kwangu Neno lake limetimizwa, Kwake sina shaka lo lote. Katika Yesu sina shaka, Ingawa nina haja; Hunifariji na upendo, Ajua kufurahisha. Kaitka Yesu sina shaka, Na ameniridhisha; Yeye tayari kuniponya, Kwake nimefadhilika.

194.YESU BWANA WANGU ANIPENDA

Yesu Bwana wangu anipenda, Nguvu zote hazitatutenga; Akatoa uzima wake, Niwe mali yake.     Yesu ni Bwana wangu,     Mimi mali yake;     Si kwa muda wa miaka tu,     Bali kwa milele. Nilipotea mbali dhambini, Yesu akaja toka mbinguni; Akanivuta na pendo lake, Niwe mali yake. Furaha tele, nimeokoka, Kutoka dhambi nimefunguka: Akaniponya kwa damu yake, Niwe mali yake.

195. MBONA HUMKUBALI MWOKOZI SASA?

Mbona humkubali Mwokozi sasa? Kwa upole akusihi; Umjie Yesu, anakungojea, Kusamehe Yu tayari.     Mbona humkubali?     Mbona? Mbona?     Usimkatae anakusihi,     Umkubali sasa. Roho hatakusihi siku zote, Umkubali Yesu sasa; Labda kesho hutapata nafasi, Usichelewe kabisa. Twae Kristo awe Mwokozi wako, Utakuwa na salama; Mambo ya kesho yajapokujia, Hutaogopa mashaka.

196. KUMJIA YESU MWOKOZI WANGU

Kumjia Yesu Mwokozi wangu, Nina Raha, Nina Raha; Nikiona shida haidhuru, Ninayo Raha.     Raha ya ajabu,     Raha yake Mungu;     Tangu mkombozi aliniokoa     Nina Raha. Amani kama bahari mpana, Nina Raha, Nina Raha; Napumzisha roho kwake Bwana, Ninayo Raha. Katika rohoni sina vita, Nina Raha, Nina Raha; Nimetakaswa, nimeokoka, Ninayo Raha.

197. MUNGU ALIAHIDI

Mungu aliahidi, Na kwa fadhili yake; Tutapata pumziko, Katika mkono wake.     Tukiona mashaka mengi,     "Tulia", amri yake,     Roho yangu ina amani,     Katika mkono wake Ijapo hufahamu, Na usifadhaike; Hutasumbuka tena, Katika mkono wake. Na ukishughulika, Kwa mambo siku zote; Roho itapumzika, Katika mkono wake. Furaha ya ajabu, Tena amani yake; Zimewekwa tayari Katika mkono wake.

198. MUNGU BABA YANGU, U MWAMINIFU

Mungu Baba yangu, U Mwaminifu, Hakuna geuzo ndani yako; Hubadiliki, wewe ndiwe sawa, Jana, leo na siku zijazo.     Wewe Mwaminifu, Wewe Mwaminifu,     Kila siku fadhili napewa;     Vitu vyote ninavyo umenipa     Wewe Mwaminifu kwangu Bwana. Na viumbe vyote hulingamana, Kuonyesha utukufu wako; Jua, na mvua, mwezi tena nyota Hulishuhudia pendo lako. Samaha la dhambi, tena amani, Hivi vyote ni baraka zako; Nguvu zako zitadumu milele, Nimebarikiwa sasa kwako.

199. MUNGU WANGU, NDIYE NAMWAMINI

Mungu wangu, ndiye namwamini, Po pote nilipo duniani; Lo lote lanijialo, Baba yangu hunitunza humo.     Namwamini Mungu hunipenda     Katika dhiki ama mashaka;     Matesoni hunilinda,     Baba yangu hunitunza sana. Mungu hulinda viumbe vyake, Huviongoza njiani mwake; Najua anikumbuka, Baba yangu hunitunza sana. Njia ijapokuwa gizani, Kodnoo hawasahauliwi; Mungu Mchunga aongoza Baba yangu hunitunza sana.

200. NAJUA JINA NILIHESHIMULO

Najua jina niliheshimulo, Lanipendeza rohoni mwangu; Jina thamani kupita hesabu, Yesu ndilo jina la ajabu.     Moyo wangu umependezwa sana,     Nikukumbukapo jina la Kristo;     Sina jina jingine liwezalo,     Kunipatia wokovu nalo. Jina hili huniletea raha, Huondoa sikitiko langu; Huimarisha aliyelemewa, Jina hilo huponya kabisa. Jina hilo litadumu milele. Nguvu zake hazibadiliki; Jina hilo linang'ara daima, Jina la Yesu halipunguki.

201. KWA MJI WA MWANGAZA

Kwa mji wa mwangaza Hapana usiku; Hautapita tena, Hapana usiku.     Mungu atayafuta     Machozi na hasara;     Hapo miaka itakoma     Hapana usiku. Jua halitakiwi Hapana usiku; Yesu ni nuru kweli, Hapana usiku. Kwa mji wa mbinguni Hapana usiku; Milele furahini, Hapana usiku.

202. ALISHUKA KUTOKA MBINGUNI

Alishuka kutoka mbinguni, Yesu Bwana wangu; Kwangu akaziondoa dhambi, Napendwa na Mungu.     Sina budi kumpenda,     Yesu Mwokozi,     Sina budi kumpenda,     Ndiye Mwokozi. Sistahili kupata neema, Neema yake mkuu; Na badala yangu akateswa, Kwa uovu wangu. Yesu yu Mwema kuliko wote, Hupenda kwa haki; Nauona utukufu wake, Na Mungu mbinguni.

203. NIKILEMEWA NA MIZIGO MINGI

Nikilemewa na mizigo mingi, Nikitembea bila tumaini; Mwokozi wangu ameniahidi, Niambie ahadi zake tena.     Niimbie ahadi tena,     Mara kwa mara ahadi tena;     Na nitafurahi, hapana huzuni,     Niambie ahadi zake tena. Nikizungukwa na hatari nyingi, Na nikishikwa na hofu moyoni; "Sitakuacha," asema Mwokozi, Niambie ahadi zake tena. Na nikiingia mbinguni kwake, Kupumzika salamani milele; Ahadi zake tamu, zikumbukwe, Niambie ahadi zake tena.

204.BWANA WANGU YU MCHUNGAJI

Bwana wangu yu mchungaji, Hunilaza chini; Kwa malisho ya majani Huniongoza mimi. Nafsi yangu huhuisha, Ananitembeza Njiani mwake kwa haki yake, Katika jina lake. Nijapopita bondeni Mwisho mwa maisha, Sitaogopa baya lo lote, Wewe upo na mimi. Wema wako na fadhili, Itanifuata Katika nyumba yake Mungu, Kutakuwa makao.

205. RAFIKI ZANGU WANATAFUTA

Rafiki zangu wanatafuta Vile vileteavyo furaha; Naijua siri kuvipata, Katika Yesu tuna anasa.     Haja yangu ni kwa Yesu,     Aridhisha kwa furaha;     Bila Yeye sitafaa,     Ndaniyake uzima. Wengine huishika mizigo Zinazolemeza na kilio; Bali tunaye Rafiki Mwema, Atakayesaidia sasa. Maskini wote wanamhitaji, Waondoke kutoka dhambini; Yesu atawaokoa kweli, Ili sasa wapate kuishi.

206. UNA NAFASI KWA YESU?

Una nafasi kwa Yesu? Aliyeondoa dhambi; Abishapo mlango wako, Umkaribishe ndani.     Nafasi kwa Mfalme Yesu,     Neno lake ulitii;     Ufungue moyo wako,     Aingie moyoni. Anasa ina nafasi, Bali Yesu hawezi; Kuingia moyo wako, Mbona wewe humpendi? Una nafasi kwa Yesu? Leo akikuita Usimkatae, mwenzangu, Ni bora kumwitika.

207. UNIFUNDISHE, EWE, BWANA

Unifundishe, Ewe, Bwana, Siku kwa siku, nakuomba; Unipe nguvu yako tele, Nguvu kushinda kwa milele. Unifundishe Bwana wangu, Kuomba kwako, kila siku; Mapenzi yako niyajue, Unipe nguvu yako tele. Unipe nguvu ya kuomba, Niwe mwaminifu daima; Nifanye kazi yako njema, Watu wakae na salama Bwana wangu unifundishe, Kuomba uniimarishe; Na nguvu yako, unijaze, Kwa fadhili, nguvu unipe.

208. KWAKE YESU, NAKAA SALAMANI

Kwake Yesu, nakaa salamani, Ijapokuwa giza na shida; Nitamwamini, atanihifadhi, Amenikomboa niwe wake. Kwake Yesu, kwake Yesu, Sitajitenga na Yeye; Kwake Yesu, hapo nadumu, Kwa salama ya milele. Kwake Yesu, ninalo kimbilio, Wakati nionapo huzuni; Ataniponya nisifadhaike, Nitakaa naye salamani. Kwake Yesu iko fuhara tele, Nitaishi naye mpaka mwisho; Atanilinda, sitashindwa kamwe, Hunipa baraka na pumziko.

209. NAFIKIRI JUU YA KALVARI

Nafikiri juu ya Kalvari, Naona watu wengi Waliomdharau Bwana wangu Alipokufa mtini. Aleluya, Aleluya, Kumbuko lenye heri; Nafikiri juu ya Kalvari; Nafikiri - fikiri juu ya Mwokozi Nafikiri juu ya Kalvari, Naona Msalaba; Na Bwana wangu akiangikwa Katikati ya wevi. Nafikiri juu ya Kalvari, Tumai la milele; Dhambi ziliondolewa hapo, Sasa ninafurahi.