208. KWAKE YESU, NAKAA SALAMANI



Kwake Yesu, nakaa salamani,

Ijapokuwa giza na shida;

Nitamwamini, atanihifadhi,

Amenikomboa niwe wake.


Kwake Yesu, kwake Yesu,

Sitajitenga na Yeye;

Kwake Yesu, hapo nadumu,

Kwa salama ya milele.


Kwake Yesu, ninalo kimbilio,

Wakati nionapo huzuni;

Ataniponya nisifadhaike,

Nitakaa naye salamani.


Kwake Yesu iko fuhara tele,

Nitaishi naye mpaka mwisho;

Atanilinda, sitashindwa kamwe,

Hunipa baraka na pumziko.

Comments

Popular posts from this blog

193. KATIKA YESU SINA SHAKA

197. MUNGU ALIAHIDI