197. MUNGU ALIAHIDI
Mungu aliahidi, Na kwa fadhili yake; Tutapata pumziko, Katika mkono wake. Tukiona mashaka mengi, "Tulia", amri yake, Roho yangu ina amani, Katika mkono wake Ijapo hufahamu, Na usifadhaike; Hutasumbuka tena, Katika mkono wake. Na ukishughulika, Kwa mambo siku zote; Roho itapumzika, Katika mkono wake. Furaha ya ajabu, Tena amani yake; Zimewekwa tayari Katika mkono wake.
Comments
Post a Comment