206. UNA NAFASI KWA YESU?



Una nafasi kwa Yesu?

Aliyeondoa dhambi;

Abishapo mlango wako,

Umkaribishe ndani.


    Nafasi kwa Mfalme Yesu,

    Neno lake ulitii;

    Ufungue moyo wako,

    Aingie moyoni.


Anasa ina nafasi,

Bali Yesu hawezi;

Kuingia moyo wako,

Mbona wewe humpendi?


Una nafasi kwa Yesu?

Leo akikuita

Usimkatae, mwenzangu,

Ni bora kumwitika.

Comments

Popular posts from this blog

193. KATIKA YESU SINA SHAKA

197. MUNGU ALIAHIDI