195. MBONA HUMKUBALI MWOKOZI SASA?



Mbona humkubali Mwokozi sasa?

Kwa upole akusihi;

Umjie Yesu, anakungojea,

Kusamehe Yu tayari.


    Mbona humkubali?

    Mbona? Mbona?

    Usimkatae anakusihi,

    Umkubali sasa.


Roho hatakusihi siku zote,

Umkubali Yesu sasa;

Labda kesho hutapata nafasi,

Usichelewe kabisa.


Twae Kristo awe Mwokozi wako,

Utakuwa na salama;

Mambo ya kesho yajapokujia,

Hutaogopa mashaka.

Comments

Popular posts from this blog

193. KATIKA YESU SINA SHAKA

197. MUNGU ALIAHIDI