194.YESU BWANA WANGU ANIPENDA



Yesu Bwana wangu anipenda,

Nguvu zote hazitatutenga;

Akatoa uzima wake,

Niwe mali yake.


    Yesu ni Bwana wangu,

    Mimi mali yake;

    Si kwa muda wa miaka tu,

    Bali kwa milele.


Nilipotea mbali dhambini,

Yesu akaja toka mbinguni;

Akanivuta na pendo lake,

Niwe mali yake.


Furaha tele, nimeokoka,

Kutoka dhambi nimefunguka:

Akaniponya kwa damu yake,

Niwe mali yake.

Comments

Popular posts from this blog

193. KATIKA YESU SINA SHAKA

197. MUNGU ALIAHIDI