207. UNIFUNDISHE, EWE, BWANA



Unifundishe, Ewe, Bwana,

Siku kwa siku, nakuomba;

Unipe nguvu yako tele,

Nguvu kushinda kwa milele.


Unifundishe Bwana wangu,

Kuomba kwako, kila siku;

Mapenzi yako niyajue,

Unipe nguvu yako tele.


Unipe nguvu ya kuomba,

Niwe mwaminifu daima;

Nifanye kazi yako njema,

Watu wakae na salama


Bwana wangu unifundishe,

Kuomba uniimarishe;

Na nguvu yako, unijaze,

Kwa fadhili, nguvu unipe.

Comments

Popular posts from this blog

193. KATIKA YESU SINA SHAKA

197. MUNGU ALIAHIDI